Thursday 11 September 2014

Sitta akomaa na Bunge la Katiba

Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta

Dodoma. Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta ‘amekomaa’ kuhakikisha Bunge Maalumu la Katiba linafanya kazi kwa kasi na kukamilisha kila kitu ifikapo tarehe yake ya mwisho, Oktoba 4, ikiwamo kupiga kura za kupitisha Katiba inayopendekezwa kazi ambayo amesema itafanywa hadi nje ya nchi kwa wajumbe watakaokuwa huko.
Sitta alilazimika kutoa matamko mawili kwa nyakati tofauti, mara ya kwanza wakati kikao cha Bunge kilipoanza jana akieleza jinsi Rasimu ya Katiba inayopendekezwa itakavyokamilika ifikapo Septemba 21 na baadaye mchana wakati akiahirisha Bunge alipotangaza mikakati ya kukusanya kura za wajumbe hadi nje ya nchi kuanzia Septemba 26, mwaka huu.
Sitta alitumia fursa hiyo kuwataka wajumbe wa Bunge hilo watakaokuwa nje ya nchi kwa matibabu au sababu nyingine kuacha mawasiliano yao ili waweze kupiga kura wakiwa hukohuko.
Alisema uongozi wa Bunge umeanza kufanya mawasiliano na balozi mbalimbali za Tanzania nje ya nchi ili wawepo watumishi wake watakaokula kiapo cha kisheria ili wasimamie upigaji kura.
Kauli za Sitta zimekuja siku moja baada ya Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) kuweka bayana makubaliano baina ya wajumbe wake na Rais Jakaya Kikwete kuwa hataongeza muda wa uhai wa Bunge hilo, hivyo litakoma Oktoba 4, mwaka huu na hakutakuwa na upigaji wa kura ya maoni kupitisha Katiba hiyo hadi baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015.
Kauli za Sitta 
Akizungumza bungeni kwa kujiamini lakini bila kugusia ratiba ya Bunge hilo iliyokuwa inafikia Oktoba 30, mwaka huu, Sitta alisema ratiba ya Bunge hilo itaendelea kama tangazo la Rais katika Gazeti la Serikali linavyosema.
GN hiyo namba 254 iliyotolewa Agosti Mosi, mwaka huu, ililiongezea Bunge hilo siku 60 ambazo zinamalizika Oktoba 4, mwaka huu baada ya siku 70 za awali kumalizika bila kupatikana katiba inayopendekezwa.
“Kwa taarifa tu na msisitizo, ni kwamba ratiba yetu ya Bunge Maalumu inaendelea kama ilivyopangwa,” alisema Sitta huku akishangilia kwa makofi na wajumbe waliokuwamo.
“Siku 60 za Bunge hili ambazo ni nyongeza ya siku tulizopewa na Rais kwa mujibu wa sheria usipohesabu siku za Jumamosi, Jumapili na sikukuu, zinaishia tarehe 4 Oktoba,” alisema Sitta.
Alisema kikao cha Kamati ya Uongozi kilichoketi juzi, kimeelezwa kuwa Bunge hilo linakwenda vizuri na kwamba Kamati ya Uandishi imejipanga kuwapatia Rasimu ya Katiba Septemba 21, mwaka huu.
“Kwa hiyo ni dhahiri kabisa kwamba lengo tulilopewa na Taifa la kutoa Katiba inayopendekezwa tutalimudu ndani ya wakati,” alisema Sitta ambaye pia ni Mbunge Urambo Mashariki (CCM) na kuongeza:

imeandikwa katka gazeti pendwa la mwananchi..Reported by sam exavery

Zitto: Sina, sipendi, wala sitegemei kufanya biashara

    
  Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe akifafanua jambo.

Ni mengi yamesemwa kuhusu mwanasiasa huyu kijana ambaye ameongoza harakati za kisiasa katika chama chake, Chadema kwa mafanikio, ingawa safari yake ndani ya chama hicho inaelekea kuishia mahali pasipo salama. Pia, ameongoza kamati muhimu za Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa mafanikio makubwa.  Katika mahojiano maalumu na gazeti hili, Zitto ana lipi la kueleza?
Swali: Hivi ukiacha siasa unatarajia kufanya shughuli gani?
Jibu: Mimi ni mchumi na mtakumbuka baada ya hoja ya Buzwagi mwaka 2007, kamati ya Jaji Bomani  (Mark) 2007/08 tulivyo-submit (wasilisha), ripoti ya Bomani iligundua kwamba sina maarifa ya kutosha kwenye uchumi wa madini, hivyo nikaamua kwenda kusoma Ujerumani Masters ya pili ya Law in Business (Shahada ya Uzamili ya Sheria za Biashara), nikiwa bado mbunge mwaka 2009/10.
Katika Masters ile andiko langu lilihusu mfumo wa kodi kwenye sekta ya madini, mafuta na gesi. Kwa hiyo nimekuwa nikifanya chambuzi mbalimbali kama huu nilioufanya leo na kutumika katika gazeti dada la Mwananchi, The Citizen kuonyesha ni kiwango gani cha mapato ambacho Tanzania itapoteza katika kipindi cha miaka 15 ya uchimbaji wa gesi, ambayo ni Dola 55 bilioni ambayo ni zaidi ya mara mbili ya uchumi wa Tanzania.
Kwa hiyo, ninashiriki katika hizo professional associations (vyama vya kitaaluma), mimi sina biashara na sijui biashara na sina interest (nia) na biashara. Kazi ninayoipenda ni kufanya chambuzi na kufundisha.
Nimeombwa na mmoja wa maprofesa Chuo Kikuu Dar es Salaam kumsaidia katika darasa lake la Masters ya International Trade, pili Chuo cha Taifa cha Masuala ya Ulinzi (National Defense College) kule Kunduchi nimehadhiri kwenye masuala haya ya madini, gesi na mafuta.
Swali: Vipi kuhusu familia, umeoa na una mtoto?
Jibu:  Nina mtoto mmoja lakini sijaoa. Mtoto wangu anaitwa Chachage na nilimwita jina hilo kwa sababu Chachage (Profesa Sethy, marehemu) alikuwa mwalimu wangu Chuo Kikuu na alifariki Julai, 2006 na mtoto wangu alizaliwa Novemba 2006.
Mimi ni mjamaa kiitikadi. Watu wangu ni kina Chachage na Profesa Issa Shivji. Tangu nikiwa chuo, Profesa Shivji anafundisha sheria, lakini most of the time (muda mwingi) niko ofisini kwake wakati mimi nilikuwa nasoma uchumi. Chachage alikuwa anafundisha sosholojia.
Sababu inayonifanya nisioe mpaka sasa ni kutotaka kuanza kujenga familia yangu wakati nina jukumu la kuhakikisha wadogo zangu wanalelewa properly (vyema).
Swali: Marehemu mama yako (Shida Salum) amewahi kukushauri kuacha siasa na ufanye kazi unayoipenda ya kufundisha, ushauri huu unauzingatia vipi?
Jibu: Mama ni mama, mama alikuwa anajua jinsi nilivyojitoa kuhakikisha Chadema inakuwa mpaka hapa ilipofikia kwa hiyo alipokuwa akiona migogoro ile na anajua kabisa kwamba these people are not fair (watu hawa hawakunitendea haki) kwa mwanangu kwa nini sasa mwanangu apoteze muda wake kwa watu ambao hawajali kazi alizofanya.
imeandikwa katika gazeti pendwa la mwananchi....reported by sam exavery.

Friday 25 July 2014

Juhudi za kutafuta amani Gaza zachacha

Juhudi za kutafuta amani Gaza zachacha

 25 Julai, 2014 - Saa 12:57 GMT
Wapalestina zaidi ya 800 wameuawa na Waisraeli 35
Israeli imeendelea kuivirumishia makombora Gaza kucha kutwa ,huku kikao cha mawaziri wa baraza la Usalama kikitarajiwa huko Marekani kujadili mapendekezo mapya ya wito wa kusitishwa mapigano kwa misingi ya kibinadamu.
Afisa wa ngazi ya juu wa umoja wa mataifa aliyeko Gaza Bob Turner, ameiambia BBC kuwa wapalestina laki moja unusu , ambao ni asilimia 8 ya idadi ya watu wa Gaza sasa wamekimbilia hifadhi kwenye shule za Umoja wa mataifa.
Idadi ya raia wa Palestina waliouawa imezidi mia nane, huku mashambulio hayo ya Israel ya angani majini na ardhini yakiingia siku ya kumi na nane.
Wanajeshi 32 na raia watatu wa Israel wameuawa katika muda huo.
Katika ukingo wa magharibi, na Jerusalem mashariki raia wawili wa Palestina wameuawa na wengine wengi kujeruhiwa wakati waandamanaji waliokuwa na hasira kuhusu mashambulio huko Gaza walipokabiliana na vikosi vya Israel.
Maandamano yaendelea Gaza kupinga mashambulizi ya Israeli
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki Moon anasema ameshtushwa na kushambuliwa kwa shule ya Umoja huo iliyopo huko Beit Hanoun, ambako mamia ya watu walifika kutafuta hifadhi.
Hata hivyo Bwana Moon na waziri wa maswala ya kigeni wa Marekani John Kerry wanaendeleza juhudi za kutafuta makubaliano ya kusitisha vita.
Kerry alikuwa Cairo kukutana na waziri wa maswala ya kigeni wa Misri Sameh Shoukry na Ban Ki-moon ambapo wanajaribu kuishinikiza Hamas kukubali mwito wa kusitisha mapigano bila ya kuishinikiza Isareli kuondoa vikosi vyake katika ukanda wa Gaza.
Wapalestina wakabiliana na polisi Gaza kupinga uvamizi wa Israeli
Israeli iliishambulia Gaza Julai tarehe 8 ikitafuta mbinu za kuzima mashambulizi ya makombora ya Hamas yanayotokea Gaza.
Mapema leo maandamano makubwa yalifanyika katika ukingo wa Magharibi mwa Palestina karibu na mpaka wake na Israel kupinga mashambulio yanayofanywa na Israel.
Waandamanaji hao wakiwa na hasira walipambana na vikosi vya usalama vya Israel.
Hata hivyo mapambano makubwa dhidi ya vikosi vya usalama ilikuwa katika eneo la Qalandia katika mpaka wa Ramallah and Jerusalem.
Habari na BBC Swahili.kwa maoni simu namba 0752-545235 Email.samexavery@yahoo.comjuhudi za kutafuta amani Gaza zachacha

Mama anayeugua Ebola atoroshwa

 25 Julai, 2014 - Saa 13:44 GMT
Mwanamke aliyeambukizwa Ebola atoroshwa Hospitalini huko Freetown
Hali ya Tahadhari imetangazwa mjini Freetown Sierra Leone baada ya mwanamke mmoja aliyeambukizwa Ebola kutoroshwa kutoka Hospitalini na jamaa zake kwa hofu kuwa angekufia huko.
Maafisa wa Usalama wa Umma na wale wa Afya wanaendelea kumtafuta wakitumia vyombo vya habari na hata redio kutangaza kuwa kuwepo kwake nje ya Hospitali na hatari kwa afya ya umma.
Mama huyo ndiye aliyekuwa wa kwanza kudhibitishwa kuugua Ebola mjini Freetown.
Mama anayeugua Ebola atoroshwa hospitalini Freetown
Wakati huohuo Mwanamume mmoja aliyekuwa anafanyiwa uchunguzi nchini Nigeria kujua iwapo anaugua ugonjwa wa Ebola ameaga dunia.
Mwanume huyo ambaye ni raia wa Liberia, aliwasili Jumapili Lagos, kupitia Togo na mara akaanza kuugua na ugonjwa unaofananishwa na Ebola.
Mgonjwa huyo alikuwa ametengwa ilikufanyiwa uchunguzi kwani hakujakuwa na mgonjwa yeyote wa Ebola nchini Nigeria licha ya Ugonjwa huo kuenea kote katika mataifa ya magharibi mwa Afrika.
Iwapo itadhibitishwa kuwa alikuwa anaugua Ebola basi yeye ndiye atakayekuwa mgonjwa wa kwanza wa Ebola nchini humo.
Zaidi ya watu 600 wamefariki kutokana na Ebola magharibi mwa Afrika tangu mwezi February.
.Mlipuko wa ugonjwa huo hatari ulianza huko Guinea na kuenea hadi Liberia na Sierra Leone.
Virusi vya ugonjwa huo husababisha uvujaji mwingi wa damu na katika zaidi ya nusu ya visa vilivyoripotiwa, waathiriwa wamefariki. Hakuna chanjo dhidi Ebola .Habari na BBC Swahili maoni namba..0752-545235 Email.samexavery@yahoo.com

Air Algerie AH5017: Abiria wote waliaga


Abiria wote na wahudumu wa ndege ya Air Algerie AH5017 waliangamia jangwani.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande ametangaza kuwa majeshi ya ufaransa yamefaulu kupata mabaki ya ndege lakini hawakuweza kuokoa nafsi hata moja.
Aidha rais Francois Hollande ametangaza kuwa majeshi hao wamepata mtambo wa kunukuu sauti ''Blackbox'' huko Mali ilikoanguka ndege hiyo iliyokuwa ikielekea mji mkuu wa Algeria Algiers.
Abiria wote wa ndege ya Air Algerie waliangamia jangwani
Ndege hiyo ilikuwa imetoka mji mkuu wa Burkina Faso Ouagadougou ikiwa na Abiria 110 na wahudumu 6 .
Abiria 51 waliokuwa ndani ya ndege hii walikuwa ni raiya wa Ufaransa.
Wengine walikuwa 27kutoka Burkina Faso, 8 kutoka Lebanon , 6 kutoka Algeria , 2 kutoka Luxembourg, 5 kutoka Canada, Wajerumani 4 .
Jamaa ya wahasiriwa wanakutana huko Ougadougu Burkina Faso
Abiria wengine walikuwa mmoja kutoka mataifa ya Cameroon , Ubeljiji ,Misri Ukraine Uswisi Mnigeria na mmoja kutoka Mali.
Waziri wa Usalama wa ndani wa Ufaransa Bernard Cazeneuve alisema ndege hiyo iliyokuwa ikielekea Algiers kutoka mji mkuu wa Burkina Faso , Ougadougou,ilianguka kutokana na hali mbaya ya anga. habari na BBC swahili. maoni simu namba..0752-545235 email.samexavery@yahoo.com

Friday 18 July 2014

TAZAMA VIDEO HII..MADHARA MAKUBWA YANAYOTOKEA KUTOKANA NA VITA NCHINI ISRAEL{GAZA}

.MADHARA MAKUBWA YANAYOTOKEA KUTOKANA NA VITA NCHINI ISRAEL{GAZA
yameripotiwa kua ni makubwa sana kiuchumi hata kijamii ambapo imeripotiwa kua majengo mengi ya yanayotomiwa kwa shughuri za kijamii nceharibiwa tazama video hii kuona baadhi ya majengo yalio halibiwa.

MASKINI GAZA.......! BOFYA HAPA CHINI KUONA VIDEO MBALIMBALI ZINAZOONYESHA VITA VINAVYO ENDELEA ISRAELI

VITA VINAVYO ENDELEA ISRAELI.ni jambo linalo huzunisha sana hususani kwa hali inayooneka kwa sasa katika nchi ya israeli na wapaletina maana wengi wao ni watoto wadogo sana wanaokufa pasipo kuwa na hatia.

ZAIDI YA WATU 20 WAMERIPOTIWA KUFA KATIKA MJI WA GAZA ISRAEL!

majeruhi kaiktka mapigano yanoyoendelea  huko nchini israel katika mjii wa gaza.                                                                                                                                                                                      Benjamin Netanyahu ameyaagi za majeshi yake kuanza kufanya uchunguzi wa chini kwa chini katika mji wa GAZA taarifa hii imetolewa na ofisi yake netanyahu, uku taarifa zaid zikisema watu 23 wanashikiliwa kwa kushukiwa kwa ugaidi na mtu mmoja kati ya ni raia wa israel.
       day into the fighting, Netanyahu is announcing a significant expansion of the ground operation.                                                                                                                                                                                                    na mnukuu.Bw. Benjamin Netanyahu
"My instructions ... are to prepare for the possibility of significantly widening the ground operation, and the military is preparing accordingly," he said in the run-up to a meeting of his cabinet ministers, according to Reuters.
                                                                                                                                                        

Sunday 13 July 2014

FULL Time 90 mints GERMANY 0-0 ARGENTINA



f

LIVE MATCH.Half Time Mints45 GERMANY 0-0 ARGENTINA


LIVE MATCH  Half Time Mints45 GERMANY 0-0 ARGENTINA

JAJI MANETO: POLISI WABEBE LAWAMA MILIPUKO YA MABOMU

SAMEXA.BLOGSPOT.COM.                                                                                    Jaji Maneto.                                                                                                     Wakati matukio ya milipuko ya mabomu yakiendelea katika baadhi ya mikoa nchini, aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu Amir Manento amelinyooshea kidole jeshi la polisi kwa madai kuwa linahusika na baadhi ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu katika vipindi tofauti nchini.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na waandishi wa Mwananchi nyumbani kwake Oysterbay juzi, alisema ingawa matukio hayo yalianza taratibu, Polisi ilishindwa kuchukua uamuzi wa haraka wa kuyazuia yasiendelee.
Aidha, alisema kuwa wakati akiwa katika Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, walifanya utafiti wa matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu, ambapo walibaini kuwa polisi walishiriki kumpiga bomu mtu mmoja na mwingine risasi katika matukio tofauti.(P.T)
"Jeshi linapofanya hayo madhambi nani ataliambia, maana polisi ni wakala wa dola (state agency)," alifafanua.
Alieleza kuwa kinachotokea hivi sasa nchini ni sawa na hadithi ya kinyonga na inzi, ambapo kinyonga huanza kumtishia inzi kwa kumshtua huku akiendelea kumsogelea taratibu na kisha hutoa ulimi haraka na kummeza.
"Tusiendelee kubaki kusema kwenye majukwaa kuwa hiyo amani itapotea, inaanza kidogo kidogo yule kinyonga alianza kurusha mguu mmoja akauweka pale chini pu! Akasikiliza, je, anaondoka? Akarusha mguu wa pili...," alifafanua zaidi.
Baadhi ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu yaliyowahi kutokea hivi karibuni ni pamoja na milipuko ya mabomu, watu kumwagiwa tindikali, uchomaji wa makanisa, utekaji nyara na mauaji ya raia kwenye mikusanyiko na kwenye maandamano ya kisiasa.
Akitoa mfano, Jaji Manento alisema katika tukio la kwanza la mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa Chadema jijini Arusha, Jeshi la Polisi lilishindwa kutekeleza wajibu wake kutokana na kusikiliza kauli za viongozi wa kisiasa.
"Viongozi fulani wa siasa wakasema wamejipiga wenyewe, badala ya kuangalia kama kuna haki za binadamu zimekiukwa. Kuna binadamu wamekufa, wamepigwa bomu, kwa hiyo inawezekana hao watu wanaoshughulikia usalama wakaacha kufanya wajibu wao wa kuangalia nani kapiga hili bomu. Wakaona imekubalika kwa sababu imeongelewa kwenye vyombo vya habari kuwa wamejipiga wenyewe.
"Kwa hivyo, siasa kwa kiasi fulani inaingizwa ingizwa...lakini sasa unakuta vile vyombo ambavyo vinatakiwa kuchunguza na kupeleleza haki za binadamu havifanyi kazi inavyopaswa ifanywe. Vyombo hivyo ni hivi vya usalama vinavyopaswa kulinda watu na mali zao," alisema.
Jaji Manento aliyewahi kuwa Jaji Kiongozi, alisema kutokana na polisi kutokuwa wazi katika kushughulikia vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, wananchi wengi wanaamini kuwa chombo hicho cha ulinzi kinahusika na matukio hayo.
"Sisemi kwamba linahusika moja kwa moja ila wananchi wataendelea kuwa na mawazo hayo, kwa sababu ya kutoelezwa ukweli. Hatua zikichukuliwa haraka, watu watafarijika, kama watu wanasema wewe ndiyo mwizi wala hukanushi, kwa hivyo watu wanaamini wewe unahusika," alisema Jaji na kuongeza:
Chanzo:Mwananch Tuma Maoni 0718192930 E-mail samexavery@yahoo.com

Wapalestina wakimbia Gaza kaskazini

Wapalestina wahama Gaza kaskaziniSAMEXA.BLOGSPOT.COM
Mamia ya Wapalestina wamekuwa wakikimbia sehemu za kaskazini za Gaza, baada ya Israel kuonya kuwa italenga sehemu hiyo katika mashambulio yake ya sasa                                                                             watu kama 4,000 tayari wameomba hifadhi katika hifadhi ya muda Jumamosi usiku mashambulio ya ndege za Israel yaliendelea Gaza.Wapalestina zaidi ya 160 wameuwawa hadi sasa.Hamas imerusha makombora zaidi dhidi ya miji ya Israel pamoja na Tel Aviv; hakuna mtu aliyekufa Israel Israil ilisema wanajeshi wane walijeruhiwa waliposhambulia eneo ambapo makombora yakirushwa.Hamas inasema wanajeshi wa Israil hawakuwahi kufika ardhini.                                                                                            Toa maoni.0718192930,E-mail samexavery@yahoo.com

Mgomo mwengine wapamba moto A. Kusini

Wanachama wa NUMSA
Mgomo mwengine wapamba moto A. Kusin                                                                                                Wachimba migodi wa Afrika Kusini wamekataa nyongeza ya mishahara iliyopendekezwa na makampuni ya Chama cha wachimba migodi, NUMSA, chama kikubwa kabisa cha wafanyakazi Afrika Kusini, piya kimetishia kuwaomba maelfu ya wafanyakazi katika sekta mbalimbali kujiunga na mgomo wao.
Wanachama wa NUMSA, katika sekta ya chuma cha pua na kutengeneza mashini walianza mgomo kama wiki mbili zilizopita - na kusababisha kiwanda kimoja cha kutengeneza zana za magari kufungwa; na kuzusha hofu kuwa uchumi wa Afrika Kusini unaweza kuzorota tena.
Mgomo huu wa sasa umeanza punde baada ya wachimba dhahabu nyeupe kurudi makazini baada ya mgomo wa miezi mitano.Tuma maoni.0718192930 E-mail samexavery@yahoo.com

Thursday 10 July 2014

Kinana-afanya-mazungumzo-na-mgombea-wa.

Kinana-afanya-mazungumzo-na-mgombea-wa.       Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mgombea wa Urais wa        Msumbiji Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi kwenye hotel ya Golden Tulip ambapo alikuwa na  .                    Katibu wa NEC Siasa na mazungumzo nayeUhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro ambaye pia ni Waziri wa Katiba na Sheria akisalimiana na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Frelimo Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi, kabla ya kuanza kwenye hoteli ya Golden Tulip . Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya Frelimo Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi akijibu baadhi ya maswali ya waandishi wa habari ambao walitaka kufahamu mahusiano yao na CCM pamoja na namna Demokrasia inavyoendeshwa nchini Msumbiji,Mheshimiwa Nyusi alisema mahusiano yao na CCM ni mazuri na ya kihistoria Tangia wakati wa mapambano ya Ukombozi,alipoulizwa kuhusu uwezo wake wa kuongea Kiswahili vizuri alisema wakati wa mapambano ya Ukombozi aliwahi ishi Tunduru na Nachingwea nchini Tanzania. Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwa pamoja na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dr.Asha-Rose Migiro(Kulia),Katibu wa NEC Oganizesheni Dr.Mohamed Seif Khatibu na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na Maofisa wengine wa Chama Cha Mapinduzi kwenye meza ya mazungumzo na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya chama cha Frelimo Mheshimiwa Filipe Jacinto Nyusi na Ujumbe wake kwenye ukumbi wa  Nyerere,Golden Tulip Hotel.

Rais-azindua-jengo-la-halmashauri-la-bil-2/-

samexa.blogsport.comjakaya-Mrisho-Kikwete_2d87f.jpg   RAIS Jakaya Kikwete jana amezindua Jengo la ofisi za Halmashauri ya wilaya ya Kilindi lililogharimu zaidi ya Sh bilioni mbili hadi kukamilika kwake.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kwa Rais Kikwete, Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Daudi Mayeji alisema jengo hilo la kisasa lina jumla ya vyumba 82 vya ofisi ikiwemo ukumbi mdogo na mkubwa.
Mayeji alisema mradi wa ujenzi wa jengo hilo la makao makuu ya Halmashauri ya wilaya hiyo ulianza rasmi mwaka 2007 baada ya serikali kutoa fedha za ujenzi.
Ujenzi ulifanywa na kampuni ya Mkandarasi AFRIQ Engeering and Construction Co. Limited, chini ya Mhandisi Mshauri National Estate Development Company Ltd (NEDCO).
Alisema katika mradi huo halmashauri hiyo ililazimika kuingia mikataba ya ujenzi wa jengo hilo kwa awamu mbili kutegemeana na upatikanaji wa fedha.
Wakati huo huo, katika kukabiliana na tatizo la maji katika kata ya Kwediboma iliyopo wilayani Kilindi serikali imetenga Sh bilioni 2.8 kwa ajili ya kukamilisha mradi wa maji safi kwenye vijiji kumi vinavyounda kata hiyo.
Rais Kikwete amebainisha hayo jana wakati akihutubia wananchi wa kata ya Kwediboma kabla ya kuzindua ujenzi wa mradi wa maji ya bomba wa kijiji cha Kwediboma unaotekelezwa kupitia mpango wa kuendeleza sekta ya maji kwa ufadhili wa Benki ya Dunia kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania.
Alisema fedha hizo zimetengwa katika bajeti ya mwaka wa fedha ujao wa 2014/2015 kusaidia kupunguza ukubwa wa tatizo la upatikanaji wa huduma hiyo kwa wananchi hasa waishio maeneo ya vijijini.
“Ndugu zangu pamoja na serikali kuwekeza fedha hizi tambueni kwamba kama jamii mnalo jukumu kubwa la kuhakikisha mradi huu unatunzwa ili uwe endelevu kwa ajili ya kutoa huduma kwenu na vizazi vijavyo...naomba wananchi waote washiriki kutimiza jukumu hili ili kutoa huduma endelevu”, alisema Rais.
Vijiji vitakavyonufaika na huduma ya maji kupitia fedha hizo ni Mpalahala, Kwedigole, Kileguru, Mzinga ambavyo kwa sasa havina huduma ya maji hasa baada ya ya chanzo chao tegemezi ambacho kilikuwa ni Malambo mawili yaliyojengwa na halmashauri kupitia mradi wa DADPS kubomolewa na mvua msimu uliopita.
Awali akisoma taarifa kuhusu mradi huo, Katibu wa Kamati ya Mradi huo Ibrahimu Abdallah alisema hadi kukamilika kwake, unatarajiwa kugharimu Sh 517,364,391 na kwamba mpaka sasa zimetumika Sh 316,197,327 kwa ajili ya kukamilisha kazi za awamu ya kwanza ya mradi.
CHANZO:HABARILEO

Tuma Maoni 0718192930,E-mail samexavery@yahoo.com

Majeruhi-wa-bomu-la-arusha-wachunguzwa.

asah-mwambene10_300_173_10da8.jpg

samexa.blogsport.com Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene
MAJERUHI wa bomu lililolipuliwa katika mgahawa wa Vama Traditional Indian Cuisine jijini Arusha juzi, wanachunguzwa na Jeshi la Polisi na Idara ya Uhamiaji.
Taarifa za awali ambazo gazeti hili lilizipata jana, zilidai tukio hilo la bomu linatokana ugomvi wa kibiashara. Taarifa hizo zilidai kuwa Jeshi la Polisi lilikuwa linaendesha uchunguzi wa tukio hilo na pamoja na madai kuwa linatokana na ugomvi wa kibiashara.(Martha Magessa)
Alipohojiwa kwa njia ya simu jana juu ya tukio hilo na madai kuwa kuna hisia linatokana na ugomvi wa kibiashara, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene alisema, “ni kweli na mimi nimesikia taarifa hizo, lakini tuviachie vyombo vya ulinzi na usalama, vilifanyie kazi tukio hilo na vitatoa taarifa kamili vikimaliza uchunguzi wao”.
Kwa upande wake, Kamanda wa Idara ya Uhamiaji Mkoa wa Arusha, Daniel Namomba, alisema jana ofisi yake inafanya uchunguzi kuhusu majeruhi wa tukio hilo, kubaini kama uwepo wao nchini ulikuwa ni wa kihalali.
Namomba alisema wanapitia nyaraka zote za majeruhi hao ili kujua kama wapo, waliokuwa wanafanya kazi hapa nchini kwa vibali maalumu; na endapo kulikuwa na watalii kati yao, ambao waliingia nchini kihalali.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jana, ofisa huyo alisema, “Siwezi kuthibitisha kama majeruhi hao walikuwa hapa nchini kihalali au la, naomba unipe muda kwa kuwa suala hili ofisi yangu inalifanyia kazi na baada ya uchunguzi kukamilika nitatoa taarifa rasmi”.
Kumekuwepo taarifa jijini hapa kwamba mfanyabiashara mwenye asili ya Asia (jina tunalo), ndiye aliyekuwa mwenyeji wa majeruhi hao, wanaodaiwa kuwa watalii, huku taarifa nyingine zikidai ni wafanyabiashara wa madini.
“Majeruhi hawa wapo ambao ni wafanyakazi hapa (Arusha) kwa zaidi ya miaka 15, lakini baadhi yao siyo raia na inadaiwa kuwa ni watalii na wengine wanadai walikuja hapa zaidi ya wiki moja iliyopita kwa lengo la kufanya biashara ya madini,” alisema mmoja wa watu, ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini.
Waziri hospitalini
Katika hatua nyingine, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Seif Rashid alitembelea majeruhi jana katika Hospitali ya Rufaa ya Seliani.
Waziri huyo alilaani vikali kitendo hicho kilichofanywa na watu ambao wanahatarisha amani ya jiji la Arusha, ambalo ni kitovu cha utalii nchini.
Alisema hali za majeruhi zinaendelea vizuri. Alisisitiza kwamba vyombo vya ulinzi na usalama, vinaendelea na uchunguzi kubaini watuhumiwa hao hatimaye wafikishwe kwenye mkono wa sheria.
Matibabu Nairobi
Waziri alisema endapo wagonjwa watasafirishwa nje ya nchi, serikali haitahusika katika matibabu yao, kwa kuwa anaamini nchini kuna hospitali zenye uwezo mkubwa wa kutibu majeruhi.
Akizungumzia hali za majeruhi hao, Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali ya Seliani, Dk Mark Jacobson ambaye ni raia wa Marekani, alisema hali za wagonjwa zinaendelea vizuri.
Lakini, alisema mmoja kati ya wagonjwa hao, ambaye ni mtoto wa miaka (13), Ritwik Khaalelwa, amepelekwa Nairobi kwa matibabu kutokana na hali yake kutoridhisha.
Aidha, alisema Deeptak Gupta aliyepoteza mguu wa kushoto, bado yuko katika chumba cha uangalizi maalumu, kutokana na maumivu makali aliyo nayo na familia yake inafanya utaratibu wa kumhamishia Nairobi kwa matibau zaidi.
Jacobson alisema wagonjwa wengine wawili wanaendelea na matibabu hospitalini hapo. Alisema watatu wameruhusiwa kwenda nyumbani baada ya majeraha waliyoyapata, kuendelea vizuri.
Mbatia ahofu
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR- Mageuzi, James Mbatia ametaka Serikali kupitia Idara yake ya Ulinzi na Usalama wa Taifa, kurudi kazini na kufanya uchunguzi wa kina juu ya milipuko ya mabomu, yanayotokea Jijini Arusha na kutoa majibu sahihi ya matukio hayo.
Mbatia, ambaye ni Mbunge wa Kuteuliwa, alisema hayo jana jijini hapa, alipozungumza na waandishi wa habari.
Alisema mashambulio hayo katika jiji la Arusha lenye vivuto vingi vya utalii, yanatisha na yanasikitisha na uchumi wa nchi unaweza kuyumba kwa matukio hayo.
Mbatia alisema Tanzania ni nchi ya pili duniani kwa kuwa na vivutio vya utalii vingi na uchumi wa nchi katika sekta ya utalii, pato lake ni sawa na asilimia 17 sawa na Sh trilioni 9.6 kwa mwaka.
Alisema watu na mali zao katika maeneo ya Jiji la Arusha na Zanzibar, wanapaswa kulindwa kwa nguvu zote.Alisema serikali inapaswa kufuatilia na kutambua adui wanayepambana naye.
Alishauri serikali na vyombo vyake vya ulinzi na usalama, kukusanya kila kiashiria cha matukio hayo bila kudharau na kisha kukaa mezani kwa kushirikisha watu mbalimbali, kuchambua kwa kina kila kimoja kupata ukweli na kisha kuufanyia kazi.
Viashiria
Alitaja baadhi ya viashiria vilivyowahi kutajwa na makundi mbalimbali kuwa ni ugomvi wa kisiasa, dini, wivu wa kibiashara ya utalii na kusherehekea na kushabikia matukio ya uvunjifu wa amani katika nchi jirani.
Vingine ni ugomvi wa marais na mgogoro wa kutaka kumng’oa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki. Alisema utaratibu wa sasa wa serikali na vyombo vya usalama, kutoa majibu mepesi kila tukio linapotokea, bila kutoa majawabu sahihi, ni dalili za kushindwa kutafutia ufumbuzi matukio hayo, hali inayoendelea kujenga hofu miongoni mwa wananchi.
Alionya kuwa serikali na vyombo vya ulinzi na usalama, haipaswi kusubiri hadi jambo litokee, ndipo ianze kupambana bali inapaswa kujipanga, ikizingatiwa tukio hilo la jana si la kwanza, bali ni la sita ndani ya kipindi cha mwaka na nusu.
Mbatia alisema alitegemea muda huu angeona anga la Arusha likiwa limefunikwa na helikopta na pia kukiwa na askari wa kutuliza ghasia mitaani.
Alisema kwa mkoa wa Arusha kuendelea kukumbwa na matukio hayo ya mabomu, kunaathiri mambo mengi, ikiwemo pato la taifa, ikizingatiwa utalii unachangia asilimia 33 ya pato la taifa. 
CHANZO:HABARILEO

Tuma Maoni 0718192930,E-mail samexavery@yahoo.com

Maoni-itafutwe-dawa-ya-utoro-baraza-la-wawakilishi.


Ssamexa.blogsport.com 
Kirusi cha utoro ambacho kimekuwa kikilitesa Bunge la Muungano wa Tanzania kwa muda mrefu, sasa kimeingia kwa kishindo kwenye Baraza la Wawakilishi (BLW), ambako shughuli za baraza hilo zimekuwa zikikwama kutokana na wajumbe kutohudhuria vikao. Hali hiyo ilijitokeza tena tangu wakati wa kikao cha kujadili bajeti ya mwaka wa fedha 2014/15 kilichoanza Mei 14, mwaka huu na kumalizika wiki iliyopi.            
Tatizo hilo la utoro wa wawakilishi wa wananchi hapa nchini awali lilidhaniwa kwamba ni la Bunge la Muungano pekee, ambako chombo hicho kwa miaka nenda miaka rudi kimekuwa kikikaa na kupitisha bajeti za Serikali na kufanya uamuzi katika mambo nyeti ya taifa pasipo kuwapo akidi, kinyume cha Katiba na Kanuni za Bunge. Udhaifu huo umekuwa tatizo sugu, kwani hata Bunge la Bajeti lililokaa mjini Dodoma kuanzia mwanzoni mwa Mei kujadili Bajeti ya mwaka 2014/15 lilimalizika wiki iliyopita likiwa limepitisha baadhi ya mambo nyeti pasipo kuwapo akidi.
Pamoja na utoro wa wabunge kwenye Bunge la Muungano kuwa tatizo sugu kiasi cha wananchi na wabunge wenyewe kuliona la kawaida, limekuwa halipigiwi kelele hata pale picha za magazeti na televisheni zinapoonyesha viti vingi bungeni vikiwa vitupu wakati vikao vya maamuzi muhimu vikiendelea. Tatizo hapa ni kukosekana vifungu katika Katiba au Kanuni za Bunge za kuwapa wananchi madaraka ya kuwawajibisha wawakilishi wao kwa kuwapigia kura ya kutokuwa na imani nao.
Hata hivyo, haikutazamiwa kwamba Baraza la Wawakilishi nalo lingekumbwa na tatizo hilo, kwani lilikuwa na mwenendo mzuri wa uwajibikaji baada ya kuanzishwa mwaka 1984 na kuendelea hivyo hadi mfumo wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK) ulipoanza baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010. Inasikitisha kwamba utoro sasa umeanza kuwa tatizo kubwa kwenye Baraza hilo, hata kuwaweka katika hali ngumu Spika Pandu Ameir Kificho, naibu wake, Ali Abdallah Ali na mwenyekiti wa Baraza hilo, Mgeni Hassan Juma kiasi cha chombo hicho kushindwa kukaa kama Kamati ya Matumizi kutokana na kutotimia akidi ya asilimia 50.
Katika tukio la wiki iliyopita, Naibu Spika Ali Abdallah Ali aliahirisha Baraza hilo kutokana na uchache wa wajumbe wakati wa kujadili bajeti ya Wizara ya Ardhi, Makazi, Maji na Nishati iliyowasilishwa na Waziri Ramadhan Abdallah Shaaban. Hivyo, Baraza hilo lisingeweza kukaa kama Kamati ya Matumizi na kupitisha vifungu kutokana na akidi ya wajumbe kutofikia asilimia 50. Tukio hilo lilitanguliwa na lile la Baraza hilo kushindwa kukaa kama Kamati ya Matumizi chini ya mwenyekiti wake, Mgeni Hassan Juma wakati wa kujadili bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko. Hiyo ni mbali na matukio mawili ya awali, wakati Spika Kificho alipoliahirisha kwa sababu ya kukosekana akidi.
Tungependa kutoa hadhari kwa wajumbe wote wa BLW kwamba vitendo vyao vya utoro siyo tu ni utovu wa nidhamu, bali pia vinahatarisha uhai wao katika Baraza hilo.
Tofauti na wapigakura wa Tanzania Bara, wenzao wa Zanzibar ni makini mno katika kufuatilia uwajibikaji wa wawakilishi wao, kwani historia imeonyesha kuwa, pamoja na kutokubali kuhongwa, hawana simile wala huruma na wawakilishi wanaowasaliti kwa kutotimiza wajibu wao.
CHANZO:MWANANACHI

Tuma Maoni 0718192930,E-mail samexavery@yahoo.com

Watu-72-wauawa-katika-mashambulizi-ya-ukanda-wa-gaza.


SAMEXA.BLOGSPORT.COM
Mashambulizi ya angani ya jeshi la Israel yameendelea usiku kucha katika Ukanda wa Gaza, na kuongeza idadi ya vifo vya Wapalestina kufikia 72 tangu mashambulizi hayo yalipoanza Jumanne wiki hii.(Martha Magessa)
Mashambulizi hayo yanawalenga wanamgambo wa Hamas katika Ukanda wa Gaza ambao nao wameyavurumisha makombora katika taifa hilo la Kiyahudi.
Mjumbe wa Palestina katika Umoja wa Mataifa, Riyad Mansoor ametoa wito wa kuitishwa kikao cha dharura cha Baraza la Usalama ili kuijadili hali hiyo.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameyaalani mashambulizi ya maroketi yanayofyatuliwa kutoka Gaza hadi Israel akisema hayakubaliki na lazima yakomeshwe.
Pia amemtaka Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kujizuia na kuheshimu wajibu wa kimataifa wa kuwalinda raia.
Ban anatarajiwa kuuhutubia mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama hii leo kuhusiana na mzozo huowa Mashariki ya Kati.
CHANZO:DW

Tuma Maoni 0718192930, E-mail samexavery@yahoo.com

Vitambulisho-vya-taifa-si-mbadala-wa-kadi-ya-mpigakura.

lubuva10_9b383.jpg
MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Damian Lubuva amesema vitambulisho vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) si mbadala wa kadi ya mpiga kura. Kauli hiyo aliitoa jana kwenye mkutano na viongozi wa vyama vya siasa alipokuwa akijibu hoja iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba aliyetaka kupata ufafanuzi wa vitambulisho vipi vitatumika kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Lipumba alinukuu kauli ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa vitambulisho vya taifa kuwa vitambulisho hivyo vingetumika kwenye shughuli za uchaguzi.
Lubuva alisema sheria iliyopo bado inatambua kadi ya mpiga kura kutumika kwenye chaguzi na kura za maoni ya katiba mpya.
“ Si kama napingana na Rais (Jakaya Kikwete), siku ile nilikuwepo na rais alikuwa akielezea faida ya kitambulisho cha taifa na kusema ‘pia vitatumika katika shughuli za uchaguzi. “Hii ina maana kama mtu kapoteza kadi ya mpiga kura, kitambulisho cha taifa kitamsaidia kutambulika. Naomba nieleweke kuwa vitambulisho vya Nida si mbadala wa kadi ya mpiga kura ila vitasaidia wakati wa uchaguzi.
Lubuva aliwataka viongozi wa vyama vya siasa kusaidia katika kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika shughuli za uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ili kazi iwe rahisi.
Hata hivyo, hoja iliibuliwa na baadhi ya viongozi wa vyama hivyo waliodai kuwapo kwa zuio la kufanya mikutano na kupendekeza muda wa uandikishwaji uongezwe. 
Chanzo:Habarileo

Tuma Maoni 0718192930 E-mail samexavery@yahoo.com

FILIKUNJOMBE KUWALIPUA BUNGENI MAKANDARASI WABOVU LUDEWA , ASIFIA KAMPUNI YA BOIMANDA

Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kushoto akishirikiana na mwananchi wa Lupingu kukata mti uliokuwepo katika njia ya kupitisha umeme kutoka Ludewa kwenda Lupingu baada ya mbunge huyo kushinda siku nzima akishiriki maendeleo ya kupeleka umeme Lupingu jumla ya vijiji 49 Ludewa kupelekewa umeme

Mbunge Filikunjombe wa pili kulia akimsikiliza mwakilishi wa meneja wa Tanroads mkoa wa Njombe Bw KIndole wakati akielezea maendeleo ya ujenzi wa barabara Ludewa 
MBUNGE wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe amepania kutumia dakika zake 15 bungeni kuwalipua makandarasi wabovu wanaoendelea na ujenzi wa barabara mbali mbali katika wilaya ya Ludewa ikiwemo barabara ya Njombe -Ludewa na Ludewa - Manda(Martha Magessa)
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo juzi wakati akikagua ujenzi wa barabara hizo katika wilaya ya Njombe na kuwa katika baadhi ya maeneo hajafurahishwa na utendaji kazi wa kampuni husika kutokana na kufanya kazi hiyo chini ya kiwango na kuwa hadi sasa ni kampuni moja pekee ambayo imeonyesha kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa .
" Serikali imewekeza mabilioni ya shilingi katika ujenzi huu wa barabara katika wilaya ya Ludewa na lengo likiwa ni kusaidia wananchi kuondokana na adha ya ubovu wa barabara .....sasa nikiwa kama mbunge mwakilishi wa wananchi nitakuwa mtu wa mwisho kufumbia macho uchakachuaji mkubwa unaofanywa na baadhi ya makandarasi hao"
Alisema hadi sasa ni kampuni moja pekee ya Boimanda ambayo imeonyesha uzalendo wa kweli katika ujenzi wa barabara kwa kiwango cha changarawe katika wilaya ya Ludewa ila makampuni yaliyosalia yamekuwa yakifanya uchakachuaji mkubwa katika ujenzi huo na kuwa zaidi ya makampuni manne ndio yanahusika na ujenzi huo kwa kila kampuni kupewa kipande.
Hivyo alisema mara baada ya kurejea bungeni kwa kikao kijacho cha bunge moja kati ya mambo ambayo atafikisha bungeni ni pamoja na shukrani kwa kampuni ya Boimanda inayoongozwa na mkurugenzi wake Nicholaus Mgaya kutokana na kuonyesha uwezo mkubwa wa kazi ila pia kufikisha kilio chake dhidi ya makandarasi wabovu wanaoendelea na ujenzi huo.
Filikunjombe alisema kasoro ambazo amepata kuziona kwa makandarasi hao ni pamoja na kujenga barabara bila kuweka mifereji ya kupita maji ,kudanganya ujazo wa kifusi kinachopaswa kumwagwa barabarani pamoja na mlazo mzuri wa barabara baada ya kuchongwa .
Kwani alisema iwapo kasoro hizo hazifanyiwa kazi basi ni wazi barabara hizo hazitadumu na baada ya mvua kunyesha ni wazi Ludewa itarejea katika kero yake ya mwanzo ya ubovu wa miundo mbinu.
Pia alisema kwa mujibu wa mikataba makandarasi hao wanapaswa kukabidhi barabara hizo tarehe 23 mwezi huu ila ukitazama ukubwa wa kazi iliyobaki ni wazi kutakuwepo na ubabaishaji mkubwa katika kumalizia kazi hiyo kwa ubora.
Wakati huo huo mbunge huyo amempongeza Rais Dr Jakaya Kikwete kwa kutekeleza ahadi yake kwa wana Ludewa juu ya uboreshaji wa barabara hizo kwa lengo la kuwezesha wawekezaji wa madini ya liganga na Nchuchuma kufanikisha kupitisha mitambo yao .
Alisema kuwa uwajibikaji wa serikali iliyopo madarakani chini ya Rais Dr Kikwete imekuwa ikileta matumaini makubwa kwa watanzania hasa wananchi wa jimbo la Ludewa ambao kwa muda mrefu sasa hawajapata kuwa na barabara za lami .
Aidha alimpongeza waziri wa ujenzi Dr John Magufuli kwa kuendelea kuwa waziri wa mfano katika baraza la mawaziri nchini kutokana na usimamizi mzuri wa miradi ya barabara japo alisema wanaoendelea kumuangusha ni makandarasi wasio wazalendo.
CHANZO:Francis Godwin

Tuma Maoni..0718192930 samexavery@yahoo.com//samexa.blogsport.com

JANGIRI SUGU LATIWA MBARONI..

WAZIRI aliyeukwaa wadhifa huo katika mabadiliko ya mwisho ya Baraza la Mawaziri yaliyofanyika mapema mwaka huu, akiongoza wizara nyeti, amebainika kuratibu mtandao wa ujangili wenye mizizi yake wilayani Manyoni na maeneo mengine mkoni Singida, vyanzo vya uhakika vya habari  vimeeleza.

Waziri huyo (jina linahifadhiwa kwa sasa) amekuwa na mawakala maalumu katika maeneo ya karibu na mapori kunakoendeshwa ujangili na mara kwa mara, hufika wilayani Manyoni kuhakiki ufanisi wa mtandao wake huo wa ujangili, huku gazeti hili likielezwa kwamba, taarifa zake ziko ‘mikononi’ mwa vyombo muhimu vya dola nchini.
Kutoka wilayani Manyoni, mkoani Singida, taarifa za ‘kiintelijensia’ zinafichua kwamba mtandao wa waziri huyo unaongozwa na mfanyabiashara (jina linahifadhiwa) wa maduka ya vifaa. Mfanyabiashara huyo ni mkazi wa kitongoji cha Mnyang’ombe mjini Manyoni na kazi zake hizo ndani ya mtandao wa ujangili huzifanya hadi mkoani Tabora.
Inadaiwa kwamba ukaribu kati ya mfanyabiashara huyo na waziri husika umejijengea nguvu zaidi kutokana na umakini wake katika kufanikisha matukio ya ujangili.
Taarifa zinabainisha kwamba mfanyabiashara huyo amekuwa na vijana maalumu ambao kazi yao ni kukusanya pembe za ndovu kutoka katika maeneo ya Itigi, Ilangali lakini katika kituo cha Manyoni, mfanyabiashara huyo hufanya kazi hiyo yeye binafsi.
Vijana hao (majina yanahifadhiwa pamoja namba zao za simu), mmoja anaishi Manyoni akimiliki namba tatu za mtandao wa aina mmoja wa simu za mkononi, mwenzake mwingine ni mwenyeji katika vijiji vinavyopakana na Pori la Akiba Rungwa, maeneo ya Kizigo. Kijana huyo wa Kizigo ndiye mnunuzi wa meno yote ya tembo yanayopatikana maeneo hayo kwa niaba ya mtandao huo.
Mbali na vijana hao wawili, yupo kijana mwingine (jina linahifadhiwa kwa sasa), huyu ni mkazi wa kijiji cha Ilangali, naye akiwa anamiliki namba tatu tofauti za simu za mtandao mmoja wa mawasiliano ya simu za mkononi. Kazi kubwa ya kijana huyu katika mgawanyo wa majukumu ya kijangili ni kuhifadhi silaha sambamba na kununua meno ya tembo kwa ‘wadau’ hapo kijiji cha Ilangali na baada ya kununua meno hayo, mfanyabiashara wa Manyoni hufika kuyachukua.
Mbinu za usafirishaji
Baada ya kazi ya ununuzi na ukusanyaji kukamilika, meno ya tembo yaliyopatikana, husafirishwa kwa njia ya reli ya kati chini ya usimamizi wa mfanyakazi mmoja wa Shirika la Reli Tanzania (jina linahifadhiwa) mwenye makazi yake mjini Morogoro.
Mfanyakazi huyo husimamia usafirishaji wa meno hayo kutoka Tabora hadi Itigi ambako hapo hupokelewa na mfanyabiashara (wa Manyoni) ambaye huyahifadhi hapo Manyoni.
Yakiwa hapo Manyoni, meno hayo huhifadhiwa kwa mmiliki wa mojawapo ya hoteli kubwa na maarufu mjini Manyoni, mwenye asili ya mikoa ya kanda ya kaskazini, ambaye yeye huwasiliana na waziri kwa ajili ya maelekezo zaidi juu ya namna ya kusafirisha meno hayo.
Taarifa za kiuchunguzi zinazidi kubainisha kwamba mara nyingi, waziri husika hufika hapo Manyoni kwa ajili ya kuchukua “mzigo” na kila anapokwenda huongozana na mwanamke mmoja, mwenye lafudhi ya watu kutoka mikoa ya kanda ya kaskazini (jina linahifadhiwa).
Mwanamke huyo ndiye hutumiwa kusafirisha meno hayo yaliyokusanywa yakiwamo ya kutoka ‘kituo’ chao cha Puma, mkoani Singida, ili hatimaye kuyafikisha wanakokubaliana yafike.
Waziri huyo anapokuwa Manyoni amekuwa na kawaida ya kuwakusanya washirika wake katika mtandao huo na wote hupata malazi yao katika moja ya hoteli kubwa na maarufu hapo Manyoni.
Wakiwa hapo Manyoni na bosi (waziri) genge hilo la kijangili hujiimarisha kiulinzi kwa kuweka watu wa kulinda hoteli husika na hata kudadisi wageni wengine wanaofika hotelini hapo.
Katika maeneo ya Singinda, mjini Puma, yupo kijana maalumu anayetumiwa na waziri huyo ambaye anatajwa kuwa na undugu wa namna fulani na mteule huyo wa Rais Kikwete. Kijana huyu hutumia namba za mitandao miwili tofauti ya simu za mkononi.
Huyu kazi yake kubwa ni kuwaunganisha wawindaji (wenyewe majangili huita wapigaji) na wakati mwingine hutokea waziri ndiye anayekusanya mzigo. Wakati uchunguzi huu ulipokuwa ukifanyika, kijana huyo alikuwa na meno ya tembo yaliyokuwa yamehifadhiwa eneo la Tinde, mkoani Shinyanga. Hata hivyo, uaminifu wa kijana huyo si mkubwa kwa sababu uchunguzi wetu umebaini wakati mwingine ‘huchota’ mzigo kiasi fulani na kuuza kinyemela bila mtandao kujua.
Kijana huyo, kati ya kazi alizowahi kufanya ni kuwaunganisha baadhi ya vijana na mwindaji kutoka Wilaya ya Igunga (jina na mawasiliano yake yanahifadhiwa). Mwindaji huyo wa Igunga anamiliki bunduki aina ya Rifle (namba inahifadhiwa) na wakati uchunguzi wa gazeti hili ukifanyika, alikuwa na vipande sita vya meno ya tembo ambavyo ni sawa na meno matatu.
Kwa wakati huo tukifanya uchunguzi, waziri husika alitoa maelekezo vijana wake wasimamishe shughuli zao kwa muda.
Huko wilayani Kahama, mkoani Shinyanga, Waziri husika anashirikiana na mtu (jina linahifadhiwa) ambaye anafanya biashara ya ng’ombe kama kinga ya kuficha shughuli zake za ujangili. Mtu huyu ni mnunuzi wa meno ya tembo na hukusanya meno yanayotoka katika mapori ya Moyowosi, Kigosi, Burigi, Biharamulo na Kimisi.
Hivi karibuni, mtu huyo amekuwa akikusanya meno ya tembo yanayotoka Moyowosi na amekuwa na wadau wake ambao ni watumishi wa serikali katika mapori ya Burigi na Biharamulo. Mtu huyo amenunuliwa na waziri husika gari aina ya Rav4, kwa ajili ya kukusanya meno ya tembo maeneo ya vijiji vinavyozunguka mapori hayo.
Katika maeneo ya Ilongelo na Ngamo, mkoani Singida, huko waziri husika anaendesha mtandao wake wa ujangili kwa kushirikiana na tajiri mmoja, mwenye asili ya Mkoa wa Simiyu ambaye naye anao mtandao mkubwa unaowahusisha vigogo kadhaa, akiwamo mmoja wa wabunge aliyepata kupigia kelele kuhusu ufisadi bungeni, zikiwamo fedha za akaunti za Uswisi, mbunge huyu ni mwenyeji wa kanda ya ziwa na ni kijana kwa umri.
Taarifa za kiuchunguzi zinabainisha kwamba meno ya tembo yanayokusanywa maeneo ya Singida, Kahama na Meatu hufikishwa katika kijiji cha Ngamo ambako waziri husika akiwa na mwanamke mmoja mkazi wa moja ya mikoa ya kaskazini ambaye ndiye mwenye jukumu la kusafirisha meno hayo.
Mtandao wa waziri huyo umejipanua zaidi katika operesheni za kijangili, ukihusisha Wilaya ya Babati, mkoani Manyara. Huko Babati, katika kijiji cha Mayoka, kuna tawi la ujangili la waziri huyo.
Msimamizi wa shughuli za kijangili eneo hilo ni mtu (jina linahifadhiwa) ambaye mara kwa mara huwapo Dodoma kila waziri husika anapokuwa huko kwa shughuli za Bunge. Huyu mtu ndiye husimamia ukusanyaji meno ya tembo kutoka maeneo ya Magugu na Mayoka, wakipata meno hayo kutoka katika Hifadhi ya Taifa Tarangire na ushoroba wa Tarangire – Manyara.
Kutokana na umahiri wa kuunganisha mitandao wa kijangili nchi nzima, waziri huyo kwa baadhi ya watu analinganishwa na pweza au buibui kutokana na kunasa na kuunda mtandao mpana.