SAMEXA.BLOGSPORT.COM
Mashambulizi
ya angani ya jeshi la Israel yameendelea usiku kucha katika Ukanda wa
Gaza, na kuongeza idadi ya vifo vya Wapalestina kufikia 72 tangu
mashambulizi hayo yalipoanza Jumanne wiki hii.(Martha Magessa)
Mashambulizi
hayo yanawalenga wanamgambo wa Hamas katika Ukanda wa Gaza ambao nao
wameyavurumisha makombora katika taifa hilo la Kiyahudi.
Mjumbe wa
Palestina katika Umoja wa Mataifa, Riyad Mansoor ametoa wito wa
kuitishwa kikao cha dharura cha Baraza la Usalama ili kuijadili hali
hiyo.
Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameyaalani mashambulizi ya maroketi
yanayofyatuliwa kutoka Gaza hadi Israel akisema hayakubaliki na lazima
yakomeshwe.
Pia amemtaka Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kujizuia na kuheshimu wajibu wa kimataifa wa kuwalinda raia.
Ban anatarajiwa kuuhutubia mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama hii leo kuhusiana na mzozo huowa Mashariki ya Kati.
CHANZO:DW