Thursday 10 July 2014

Vitambulisho-vya-taifa-si-mbadala-wa-kadi-ya-mpigakura.

lubuva10_9b383.jpg
MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa, Damian Lubuva amesema vitambulisho vinavyotolewa na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) si mbadala wa kadi ya mpiga kura. Kauli hiyo aliitoa jana kwenye mkutano na viongozi wa vyama vya siasa alipokuwa akijibu hoja iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba aliyetaka kupata ufafanuzi wa vitambulisho vipi vitatumika kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Lipumba alinukuu kauli ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa wakati wa uzinduzi wa vitambulisho vya taifa kuwa vitambulisho hivyo vingetumika kwenye shughuli za uchaguzi.
Lubuva alisema sheria iliyopo bado inatambua kadi ya mpiga kura kutumika kwenye chaguzi na kura za maoni ya katiba mpya.
“ Si kama napingana na Rais (Jakaya Kikwete), siku ile nilikuwepo na rais alikuwa akielezea faida ya kitambulisho cha taifa na kusema ‘pia vitatumika katika shughuli za uchaguzi. “Hii ina maana kama mtu kapoteza kadi ya mpiga kura, kitambulisho cha taifa kitamsaidia kutambulika. Naomba nieleweke kuwa vitambulisho vya Nida si mbadala wa kadi ya mpiga kura ila vitasaidia wakati wa uchaguzi.
Lubuva aliwataka viongozi wa vyama vya siasa kusaidia katika kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika shughuli za uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura ili kazi iwe rahisi.
Hata hivyo, hoja iliibuliwa na baadhi ya viongozi wa vyama hivyo waliodai kuwapo kwa zuio la kufanya mikutano na kupendekeza muda wa uandikishwaji uongezwe. 
Chanzo:Habarileo

Tuma Maoni 0718192930 E-mail samexavery@yahoo.com

No comments:

Post a Comment