Sunday 13 July 2014

JAJI MANETO: POLISI WABEBE LAWAMA MILIPUKO YA MABOMU

SAMEXA.BLOGSPOT.COM.                                                                                    Jaji Maneto.                                                                                                     Wakati matukio ya milipuko ya mabomu yakiendelea katika baadhi ya mikoa nchini, aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji Mstaafu Amir Manento amelinyooshea kidole jeshi la polisi kwa madai kuwa linahusika na baadhi ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu katika vipindi tofauti nchini.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na waandishi wa Mwananchi nyumbani kwake Oysterbay juzi, alisema ingawa matukio hayo yalianza taratibu, Polisi ilishindwa kuchukua uamuzi wa haraka wa kuyazuia yasiendelee.
Aidha, alisema kuwa wakati akiwa katika Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, walifanya utafiti wa matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu, ambapo walibaini kuwa polisi walishiriki kumpiga bomu mtu mmoja na mwingine risasi katika matukio tofauti.(P.T)
"Jeshi linapofanya hayo madhambi nani ataliambia, maana polisi ni wakala wa dola (state agency)," alifafanua.
Alieleza kuwa kinachotokea hivi sasa nchini ni sawa na hadithi ya kinyonga na inzi, ambapo kinyonga huanza kumtishia inzi kwa kumshtua huku akiendelea kumsogelea taratibu na kisha hutoa ulimi haraka na kummeza.
"Tusiendelee kubaki kusema kwenye majukwaa kuwa hiyo amani itapotea, inaanza kidogo kidogo yule kinyonga alianza kurusha mguu mmoja akauweka pale chini pu! Akasikiliza, je, anaondoka? Akarusha mguu wa pili...," alifafanua zaidi.
Baadhi ya matukio ya ukiukwaji wa haki za binadamu yaliyowahi kutokea hivi karibuni ni pamoja na milipuko ya mabomu, watu kumwagiwa tindikali, uchomaji wa makanisa, utekaji nyara na mauaji ya raia kwenye mikusanyiko na kwenye maandamano ya kisiasa.
Akitoa mfano, Jaji Manento alisema katika tukio la kwanza la mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa Chadema jijini Arusha, Jeshi la Polisi lilishindwa kutekeleza wajibu wake kutokana na kusikiliza kauli za viongozi wa kisiasa.
"Viongozi fulani wa siasa wakasema wamejipiga wenyewe, badala ya kuangalia kama kuna haki za binadamu zimekiukwa. Kuna binadamu wamekufa, wamepigwa bomu, kwa hiyo inawezekana hao watu wanaoshughulikia usalama wakaacha kufanya wajibu wao wa kuangalia nani kapiga hili bomu. Wakaona imekubalika kwa sababu imeongelewa kwenye vyombo vya habari kuwa wamejipiga wenyewe.
"Kwa hivyo, siasa kwa kiasi fulani inaingizwa ingizwa...lakini sasa unakuta vile vyombo ambavyo vinatakiwa kuchunguza na kupeleleza haki za binadamu havifanyi kazi inavyopaswa ifanywe. Vyombo hivyo ni hivi vya usalama vinavyopaswa kulinda watu na mali zao," alisema.
Jaji Manento aliyewahi kuwa Jaji Kiongozi, alisema kutokana na polisi kutokuwa wazi katika kushughulikia vitendo vya ukiukwaji wa haki za binadamu, wananchi wengi wanaamini kuwa chombo hicho cha ulinzi kinahusika na matukio hayo.
"Sisemi kwamba linahusika moja kwa moja ila wananchi wataendelea kuwa na mawazo hayo, kwa sababu ya kutoelezwa ukweli. Hatua zikichukuliwa haraka, watu watafarijika, kama watu wanasema wewe ndiyo mwizi wala hukanushi, kwa hivyo watu wanaamini wewe unahusika," alisema Jaji na kuongeza:
Chanzo:Mwananch Tuma Maoni 0718192930 E-mail samexavery@yahoo.com

No comments:

Post a Comment