Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe akifafanua jambo.
Ni mengi yamesemwa kuhusu mwanasiasa huyu kijana ambaye ameongoza harakati za kisiasa katika chama chake, Chadema kwa mafanikio, ingawa safari yake ndani ya chama hicho inaelekea kuishia mahali pasipo salama. Pia, ameongoza kamati muhimu za Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa mafanikio makubwa. Katika mahojiano maalumu na gazeti hili, Zitto ana lipi la kueleza?
Swali: Hivi ukiacha siasa unatarajia kufanya shughuli gani?
Jibu: Mimi ni mchumi na
mtakumbuka baada ya hoja ya Buzwagi mwaka 2007, kamati ya Jaji Bomani
(Mark) 2007/08 tulivyo-submit (wasilisha), ripoti ya Bomani iligundua
kwamba sina maarifa ya kutosha kwenye uchumi wa madini, hivyo nikaamua
kwenda kusoma Ujerumani Masters ya pili ya Law in Business (Shahada ya
Uzamili ya Sheria za Biashara), nikiwa bado mbunge mwaka 2009/10.
Katika Masters ile andiko langu lilihusu mfumo wa
kodi kwenye sekta ya madini, mafuta na gesi. Kwa hiyo nimekuwa nikifanya
chambuzi mbalimbali kama huu nilioufanya leo na kutumika katika gazeti
dada la Mwananchi, The Citizen kuonyesha ni kiwango gani cha mapato
ambacho Tanzania itapoteza katika kipindi cha miaka 15 ya uchimbaji wa
gesi, ambayo ni Dola 55 bilioni ambayo ni zaidi ya mara mbili ya uchumi
wa Tanzania.
Kwa hiyo, ninashiriki katika hizo professional
associations (vyama vya kitaaluma), mimi sina biashara na sijui biashara
na sina interest (nia) na biashara. Kazi ninayoipenda ni kufanya
chambuzi na kufundisha.
Nimeombwa na mmoja wa maprofesa Chuo Kikuu Dar es
Salaam kumsaidia katika darasa lake la Masters ya International Trade,
pili Chuo cha Taifa cha Masuala ya Ulinzi (National Defense College)
kule Kunduchi nimehadhiri kwenye masuala haya ya madini, gesi na mafuta.
Swali: Vipi kuhusu familia, umeoa na una mtoto?
Jibu: Nina mtoto mmoja lakini
sijaoa. Mtoto wangu anaitwa Chachage na nilimwita jina hilo kwa sababu
Chachage (Profesa Sethy, marehemu) alikuwa mwalimu wangu Chuo Kikuu na
alifariki Julai, 2006 na mtoto wangu alizaliwa Novemba 2006.
Mimi ni mjamaa kiitikadi. Watu wangu ni kina
Chachage na Profesa Issa Shivji. Tangu nikiwa chuo, Profesa Shivji
anafundisha sheria, lakini most of the time (muda mwingi) niko ofisini
kwake wakati mimi nilikuwa nasoma uchumi. Chachage alikuwa anafundisha
sosholojia.
Sababu inayonifanya nisioe mpaka sasa ni kutotaka
kuanza kujenga familia yangu wakati nina jukumu la kuhakikisha wadogo
zangu wanalelewa properly (vyema).
Swali: Marehemu mama yako (Shida Salum)
amewahi kukushauri kuacha siasa na ufanye kazi unayoipenda ya
kufundisha, ushauri huu unauzingatia vipi?
Jibu: Mama ni mama, mama alikuwa
anajua jinsi nilivyojitoa kuhakikisha Chadema inakuwa mpaka hapa
ilipofikia kwa hiyo alipokuwa akiona migogoro ile na anajua kabisa
kwamba these people are not fair (watu hawa hawakunitendea haki) kwa
mwanangu kwa nini sasa mwanangu apoteze muda wake kwa watu ambao
hawajali kazi alizofanya.
imeandikwa katika gazeti pendwa la mwananchi....reported by sam exavery.
imeandikwa katika gazeti pendwa la mwananchi....reported by sam exavery.
No comments:
Post a Comment