Dodoma. Mwenyekiti wa Bunge Maalumu la Katiba, Samuel Sitta
‘amekomaa’ kuhakikisha Bunge Maalumu la Katiba linafanya kazi kwa kasi
na kukamilisha kila kitu ifikapo tarehe yake ya mwisho, Oktoba 4,
ikiwamo kupiga kura za kupitisha Katiba inayopendekezwa kazi ambayo
amesema itafanywa hadi nje ya nchi kwa wajumbe watakaokuwa huko.
Sitta alilazimika kutoa matamko mawili kwa nyakati
tofauti, mara ya kwanza wakati kikao cha Bunge kilipoanza jana akieleza
jinsi Rasimu ya Katiba inayopendekezwa itakavyokamilika ifikapo
Septemba 21 na baadaye mchana wakati akiahirisha Bunge alipotangaza
mikakati ya kukusanya kura za wajumbe hadi nje ya nchi kuanzia Septemba
26, mwaka huu.
Sitta alitumia fursa hiyo kuwataka wajumbe wa
Bunge hilo watakaokuwa nje ya nchi kwa matibabu au sababu nyingine
kuacha mawasiliano yao ili waweze kupiga kura wakiwa hukohuko.
Alisema uongozi wa Bunge umeanza kufanya
mawasiliano na balozi mbalimbali za Tanzania nje ya nchi ili wawepo
watumishi wake watakaokula kiapo cha kisheria ili wasimamie upigaji
kura.
Kauli za Sitta zimekuja siku moja baada ya Kituo
cha Demokrasia Tanzania (TCD) kuweka bayana makubaliano baina ya wajumbe
wake na Rais Jakaya Kikwete kuwa hataongeza muda wa uhai wa Bunge hilo,
hivyo litakoma Oktoba 4, mwaka huu na hakutakuwa na upigaji wa kura ya
maoni kupitisha Katiba hiyo hadi baada ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 2015.
Kauli za Sitta
Akizungumza bungeni kwa kujiamini lakini bila
kugusia ratiba ya Bunge hilo iliyokuwa inafikia Oktoba 30, mwaka huu,
Sitta alisema ratiba ya Bunge hilo itaendelea kama tangazo la Rais
katika Gazeti la Serikali linavyosema.
GN hiyo namba 254 iliyotolewa Agosti Mosi, mwaka
huu, ililiongezea Bunge hilo siku 60 ambazo zinamalizika Oktoba 4, mwaka
huu baada ya siku 70 za awali kumalizika bila kupatikana katiba
inayopendekezwa.
“Kwa taarifa tu na msisitizo, ni kwamba ratiba
yetu ya Bunge Maalumu inaendelea kama ilivyopangwa,” alisema Sitta huku
akishangilia kwa makofi na wajumbe waliokuwamo.
“Siku 60 za Bunge hili ambazo ni nyongeza ya siku
tulizopewa na Rais kwa mujibu wa sheria usipohesabu siku za Jumamosi,
Jumapili na sikukuu, zinaishia tarehe 4 Oktoba,” alisema Sitta.
Alisema kikao cha Kamati ya Uongozi kilichoketi
juzi, kimeelezwa kuwa Bunge hilo linakwenda vizuri na kwamba Kamati ya
Uandishi imejipanga kuwapatia Rasimu ya Katiba Septemba 21, mwaka huu.
“Kwa hiyo ni dhahiri kabisa kwamba lengo
tulilopewa na Taifa la kutoa Katiba inayopendekezwa tutalimudu ndani ya
wakati,” alisema Sitta ambaye pia ni Mbunge Urambo Mashariki (CCM) na
kuongeza:
imeandikwa katka gazeti pendwa la mwananchi..Reported by sam exavery
No comments:
Post a Comment