Tuesday 8 July 2014

WAZIRI MAGUFULI AZINDUA KIVUKO MKOANI MARA.

Waziri wa Ujenzi, Dkt. John P. Magufuli amewataka wakazi wa Iramba na Majita kutunza kivuko kipya cha MV Mara ili kiweze kuwasaidia katika kuinua uchumi wa maeneo hayo.

Waziri Magufuli alitoa tamko hilo jana kabla ya kuzindua kivuko hicho kipya katika kijiji cha Iramba wilayani Bunda mkoani Mara. “Ndugu zangu wa Iramba kitunzeni kivuko hiki kwani ni mkombozi mkubwa katika kuwaletea maendeleo yenu pamoja na maeneo ya jirani” Alisema Waziri Magufuli Pia Waziri Magufuli aliwaasa wavuvi kutotega nyavu kwenye njia za kivuko ili kiweze kudumu kwa muda mrefu kwani kwa kufanya hivyo watasababisha injini za kivuko hicho kuharibika mapema.

Aidha Waziri Magufuli aliwapongeza Mbunge wa Mwibara Kangi Lugora pamoja na Mbunge wa Musoma vijijini Nimrodi Mkono kwa juhudi zao zilizochochea kupatikana kwa kivuko hicho.

Aidha, Dkt. Magufuli alisema kuwa kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba tani 25, yaani magari manne 4 na abiria 50, kitaokoa maisha ya wananchi wengi ambao walikuwa wanapata adha kubwa ya usafiri kutokana na kukosa usafiri wa uhakika ambao ulikuwa unahatarisha maisha yao.

“Nimeambiwa hapa nauli ilikuwa Shilingi 2000/= kuvuka upande wa pili kwa kutumia boti za watu binafsi lakini kwa kivuko hiki natangaza rasmi kuwa nauli kwa kivuko chetu kipya ni shilingi 500/= tu, na wanafunzi waliovaa sare watapanda bure, watoto sh.100” Alisema Waziri Magufuli. Dkt.Magufuli aliongeza kuwa nauli za magari na mizigo zitapangwa na Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA ambao ndio wasimamizi wa kivuko hicho.

Aidha, Waziri Magufuli aliongeza kuwa Serikali itaendelea kuboresha miundombinu bila kuangalia itikadi zozote za kisiasa. Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa kijiji cha Iramba, walisema kuwa walikuwa wanapa taabu sana ya usafiri kwani ilikuwa inawalazimu kuvuka kwa mitumbwi ambayoilikuwa inahatarisha maisha ya wakazi wa maeneo hayo.                                                   
Waziri wa Ujenzi, Dkt. John P. Magufuli amewataka wakazi wa Iramba na Majita kutunza kivuko kipya cha MV Mara ili kiweze kuwasaidia katika kuinua uchumi wa maeneo hayo.

Waziri Magufuli alitoa tamko hilo jana kabla ya kuzindua kivuko hicho kipya katika kijiji cha Iramba wilayani Bunda mkoani Mara. “Ndugu zangu wa Iramba kitunzeni kivuko hiki kwani ni mkombozi mkubwa katika kuwaletea maendeleo yenu pamoja na maeneo ya jirani” Alisema Waziri Magufuli Pia Waziri Magufuli aliwaasa wavuvi kutotega nyavu kwenye njia za kivuko ili kiweze kudumu kwa muda mrefu kwani kwa kufanya hivyo watasababisha injini za kivuko hicho kuharibika mapema.

Aidha Waziri Magufuli aliwapongeza Mbunge wa Mwibara Kangi Lugora pamoja na Mbunge wa Musoma vijijini Nimrodi Mkono kwa juhudi zao zilizochochea kupatikana kwa kivuko hicho.

Aidha, Dkt. Magufuli alisema kuwa kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba tani 25, yaani magari manne 4 na abiria 50, kitaokoa maisha ya wananchi wengi ambao walikuwa wanapata adha kubwa ya usafiri kutokana na kukosa usafiri wa uhakika ambao ulikuwa unahatarisha maisha yao.

“Nimeambiwa hapa nauli ilikuwa Shilingi 2000/= kuvuka upande wa pili kwa kutumia boti za watu binafsi lakini kwa kivuko hiki natangaza rasmi kuwa nauli kwa kivuko chetu kipya ni shilingi 500/= tu, na wanafunzi waliovaa sare watapanda bure, watoto sh.100” Alisema Waziri Magufuli. Dkt.Magufuli aliongeza kuwa nauli za magari na mizigo zitapangwa na Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA ambao ndio wasimamizi wa kivuko hicho.

Aidha, Waziri Magufuli aliongeza kuwa Serikali itaendelea kuboresha miundombinu bila kuangalia itikadi zozote za kisiasa. Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wakazi wa kijiji cha Iramba, walisema kuwa walikuwa wanapata taabu sana ya usafiri kwani ilikuwa inawalazimu kuvuka kwa mitumbwi ambayo ilikuwa inahatarisha maisha ya wakazi wa maeneo hayo.

No comments:

Post a Comment